Hatua za Kuomba Mikopo

  1. Maombi yote ya mikopo lazima yaidhinishwe na kamati ya mikopo;
  2. Kamati ya mikopo itaruhusu mkopo kutolewa baada ya kujiridhisha kwamba hazina itabaki salama baada ya kutoa mkopo unaoombwa;
  3. Kamati ya mikopo itahakiki rehani inayowekwa kulingana na vigezo na masharti ya mikopo kabla ya kuwasilisha ombi kwa mtunza hazina au meneja wa TCRA SACCOS kufanya malipo;
  4. Maamuzi ya kukubali au kukataa ombi la mkopo ni jukumu la kamati ya mikopo. Maelezo yatatolewa juu ya uamuzi kwenye kikao cha kamati kifuatacho;
  5. Mwanachama anaweza kukata rufaa juu ya ombi lake linalokataliwa kwa mwenyekiti wa kamati ya mikopo. Mwenyekiti na kamati ya mikopo watalipitia ombi tena na kutoa uamuzi wa mwisho;
  6. Mikopo itapitiwa na kamati mara mbili kila mwezi. Mabadiliko ya ratiba yanaruhusiwa kulingana na uhitaji, na maombi ya katibu mkuu au meneja wa TCRA SACCOS. Mabadiliko lazima yaidhinishwe na kamati ya mikopo;
  7. Utaratibu utakaotumika katika utoaji wa mikopo ni aliyeomba kwanza kupewa kwanza (FIRST COME FIRST SERVED BASIS).
  8. Mwanachama ataomba mkopo kutumia form ya mikopo.

Makubaliano ya Maombi ya Mkopo

  1. Mikopo itatolewa kwa wanachama waliokidhi vigezo na masharti ya mikopo;
  2. Kiasi kinachokopweshwa hakitazidi mara ya tatu (3) ya mchango wa mwanachama anayeomba;
  3. Kipindi cha marejesho kinaanza kati ya miezi sita (6) au thelathini na sita (36) baada ya mwanachama kupokea mkopo kuruhusu mzunguko mzuri wa pesa kulingana na aina ya mkopo;
  4. Hatua za awali za ombi la mkopo zitafuatiliwa na afisa wa mikopo na mhasibu wa TCRA SACCOS kabla ya kuwasilisha ombi hilo kwa kamati ya mikopo;
  5. Maombi yote yatafanyika kutumia fomu maalum. Kila fomu inabidi ionyeshe:
    • Kiasi kinachoombwa;
    • Madhumuni ya mkopo;
    • Muda wa marejesho uliobaki (kama mwanachama alikua na mikopo mingine);
    • Rehani;
    • Kiasi kitakachokatwa kwenye mshahara kila mwezi.
  6. Mwanachama anaweza kuchukua mkopo wenye thamani ya hadi mara tatu (3) ya mchango wake kwenye SACCOS au kulingana na uwezo wake wa kulipa marejesho;
  7. Mikopo ya maendeleo itaidhinishwa na kamati ya mikopo kuanza na mwombaji aliyeomba wa kwanza;
  8. Riba itatozwa kila mwezi kulingana na kiasi cha mkopo ambacho hakijarejeshwa;
  9. Mkopo unapotolewa, makubaliano ya mkopo yatasainiwa yakieleza ratiba ya marejesho, riba, muda wa kurejesha, na siku ya kuanza. Baada ya hapo, pesa itapewa kwa mwanachama;
  10. Kila mwaka bodi itachagua wajumbe wa kamati ya mikopo kuruhusu kila mjumbe wa bodi kua na nafasi ya kua mwanakamati ya mikopo.