Mwanzo
Historia ya TCRA SACCOS ilianza tarehe 21/04/2006 pale watumishi wa TCRA walipoanzisha umoja wa kusaidiana Mamlaka ya Mawasiliano kwa kifupi MKM. Kutokana na MKM kufanya vizuri ikaonekana haja ya kupiga hatua moja zaidi ya kuanzisha chombo ambacho kingewasaidia wanachama wake kujiletea Maendeleo.
Tarehe 08/11/2008 ulifanyika Mkutano uliotoa maamuzi ya kuanzisha SACCOS, Mchakato ulianza na tarehe 5/4/2011 TCRA SACCOS ilisajiliwa kwa namba DSR 1314. Baada ya kusajiliwa uchaguzi wa kwanza ulifanyika tarehe 20/04/2012 ambapo Ndugu Erasmo Mbilinyi alichaguliwa kuwa Mwenyekiti,Ndugu Richard Kayombo Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa Bodi ni Ndugu Abel John, Ndugu Abdul Hussein, Ndugu Massai J.Massai, Mama Doris Saivoiye na Ndugu Benjamin Mwandete.
Idadi ya wanachama ilikua 214 ambao wamengezeka hadi July 2021 ni 11, jumla ikkiwa wanachama 225.
Malengo
Malengo ya MKM pamoja na mambo mengine ilikua ni kukusanya nguvu za kifedha miongoni mwa wanachama wake ili kushirikiana katika matatizo mbalimbali kama vile misiba, magonjwa na majanga. Kutokana na MKM kufanya vizuri, ikaonekaa haja ya kuanzisha chombo kingine ambacho kingewasaidia wanachama wake kujiletea maendeleo ya kiuchumi. Chombo hicho si kingine, bali ni TCRA SACCOS.