Mwanachama wa TCRA SACCOS atakua na haki zifuatazo:

  1. Kushiriki kwenye kazi za SACCOS kulingana na sheria za uendeshaji wa shughuli za SACCOS, na makubaliano kutoka kikao kikuu cha mwaka;
  2. Kushiriki na kuchangia mawazo kwenye mikutano ya SACCOS;
  3. Kumchagua na kuchaguliwa kama kiongozi. Uchaguzi kwenye ngazi yoyote ya SACCOS utafuata vigezo vya cheo husika;
  4. Kuweka na kutoa kwenye akiba yake ya SACCOS kuzingatia kanuni na sheria za SACCOS;
  5. Kua mdhamini wa mkopo kwa mwanachama yeyote wa TCRA SACCOS;
  6. Kujulishwa kuhusu maendeleo ya TCRA SACCOS na maadhimio ya kikao kikuu cha mwaka;
  7. Kupokea gawio, kupitia vitabu vya uhasibu, mihutasari ya vikao na nakala zinginezo katika mida kawaida ya kazi;
  8. Kupewa mikopo kulingana na sheria na kanuni za TCRA SACCOS, pamoja na sera za mikopo;
  9. Kuomba kuitishwa kwa kikao cha wanachama kama isemavyo kwenye kanuni za TCRA SACCOS;
  10. Kupokea gawio kama inavyokubaliwa kwenye mikutano ya SACCOS;
  11. Mtu yeyote ambaye ataacha kua mwanachama wa SACCOS, na hana deni lolote, ana haki ya kupokea hisa zake, fedha na haki zingine zozote baada ya siku tisini (90) ya kusitisha uanachama. Gawio lolote la ziada litaweza kulipwa baada ya vitabu vya fedha kupitiwa na mkaguzi wa nje;
  12. Kuchagua mrithi.