TCRA SACCOS inatoa mikopo ifuatayo:

Mikopo ya Maendeleo

Mara kwa mara kwenye ukuaji wa biashara na familia, kuna uhitaji wa pesa za ziada kufanikisha malengo kwa wakati timilifu. TCRA SACCOS iko Pamoja nawe kukusaidia kufanikisha ndoto zako kua hai.

________________________________________

Mikopo ya Elimu

Kuwezesha masomo ya elimu ya juu, TCRA SACCOS inasaidia wanachama kuweza kufanya malipo ya ada kwa mkupuo ili kupunguza changamoto za upatikanaji wa fedha za kuongeza ujuzi na kuboresha utashi wa kazi za wanachama na familia zao.

________________________________________

Mikopo ya Dharura

Hii mikopo inalenga kusaidia wanachama pindi wamekutwa na dharura (emergency) zinazohitaji uwezo wa ziada kusuluhisha. Hii mikopo ni muhimu katika jamii yetu ili kupunguza makali ya changamoto inayomkuta mwanachama mwenzetu.

________________________________________

Mikopo ya Makazi na Nyumba

Nyumba nzuri ni fahari ya wanachama na familia zao kuweza kuishi na kukua ppamoja na jamii inayotuzunguka. TCRA SACCOS inawawezesha wanachama kujenga na kumiliki nyumba ya ndoto zao kwa mkopo.

________________________________________

Mikopo ya Kuanzisha au Kuendeleza Biashara

Iwapo mwanachama anahitaji kuanzisha au kukuza biashara, mtaji haupaswi kua kikwazo kwa mwanachama kuweza kujikwamua kiuchumi. Mikopo hii ni rafiki zaidi ya mikopo kutoka taasisi za kifedha nyingine, hivyo mwanachama atapata unafuu zaidi kwenye marejesho na kuweza kukua kwa kasi zaidi.

________________________________________

Mikopo Maalum

Kuna uwezekano kwamba aina ya mkopo unaohitajika na mwanachama haupo kwenye mikopo ya kawaida inayofahamika. TCRA SACCOS inaelewa kwamba mazingira ya namna hii yanaweza kutokea, na hivyo tunaruhusu maongezi na wanachama kuelewa zaidi kuhusu aina ya mikopo wanayohitaji kuhakikisha kwamba malengo yao yanatimia kikamilifu.