Majukumu ya TCRA SACCOS kwa Wanachama

TCRA SACCOS inafanya kazi zifuatazo:

 1. Kupokea michango na marejesho kutoka kwa wanachama;
 2. Kutoa mikopo kwa wanachama;
 3. Kuhamasisha watu kujiunga na TCRA SACCOS;
 4. Kukuza mfuko wa SACCOS kwa:
  • Kuwezesha wanachama kuongeza mchango wao kwenye SACCOS mara kwa mara;
  • Kuboresha miradi ya wanachama inayoweza kuleta faida kama ilivyokubalika kwenye kikao kikuu cha mwaka;
  • Uwekezaji kwenye taasisi za fedha, na vifungo vya hazina baada ya kutenga fedha za kukopesha;
  • Kukuza kazi zenye manufaa kwa wanachama kama ilivyokubalika kwenye kikao kikuu cha mwaka, na baada ya kupata ruhusa kutoka ofisi ya usajili wa SACCOS.