Sifa za Mwanachama

Wanachama wanapaswa kua na sifa zifuatazo:

  1. Mfanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania and ndugu wa mfanyakazi;
  2. Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa TCRA;
  3. Mfanyakazi wa zamani wa TCRA;
  4. Kikundi cha wanachama wa TCRA SACCOS.

Wanachama wapya kutoka (B) and (C), baada ya kukamilisha usajili, mwanachama mpya atakua na wajibu wa kuzingatia haki na majukumu ya wanachama.

Ustahiki wa Mwanachama

Yeyote anayetaka kujiunga na TCRA SACCOS lazima awe na yafuatayo;

  1. Umri wa miaka 18 (kumi na nane)au zaidi;
  2. Awe muaminifu mwenye utimamu wa akili;
  3. Lazima alipe kiingilio, awe na hisa, na mchango wa kwanza kulingana na kanuni za SACCOS;
  4. Aweze kutekeleza wajibu wake kama mwanachama wa TCRA SACCOS.
  5. Akubali kufuata kanuni za TCRA SACCOS na Cooperative Societies Act No.20 ya mwaka 2003.