Mwanzo

Historia ya TCRA SACCOS ilianza tarehe 21/04/2006 pale watumishi wa TCRA walipoanzisha umoja wa kusaidiana Mamlaka ya Mawasiliano kwa kifupi MKM. Kutokana na MKM kufanya vizuri ikaonekana haja ya kupiga hatua moja zaidi ya kuanzisha chombo ambacho kingewasaidia wanachama wake kujiletea Maendeleo.

Tarehe 08/11/2008 ulifanyika Mkutano uliotoa maamuzi ya kuanzisha SACCOS, Mchakato ulianza na tarehe 5/4/2011 TCRA SACCOS ilisajiliwa kwa namba DSR 1314. Baada ya kusajiliwa uchaguzi wa kwanza ulifanyika tarehe 20/04/2012 ambapo Ndugu Erasmo Mbilinyi alichaguliwa kuwa Mwenyekiti,Ndugu Richard Kayombo Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa Bodi ni Ndugu Abel John, Ndugu Abdul Hussein, Ndugu Massai J.Massai, Mama Doris Saivoiye na Ndugu Benjamin Mwandete.

Idadi ya wanachama ilikua 214 ambao wamengezeka hadi July 2021 ni 11, jumla ikkiwa wanachama 225.

Malengo

Malengo ya MKM pamoja na mambo mengine ilikua ni kukusanya nguvu za kifedha miongoni mwa wanachama wake ili kushirikiana katika matatizo mbalimbali kama vile misiba, magonjwa na majanga. Kutokana na MKM kufanya vizuri, ikaonekaa haja ya kuanzisha chombo kingine ambacho kingewasaidia wanachama wake kujiletea maendeleo ya kiuchumi. Chombo hicho si kingine, bali ni TCRA SACCOS.

Viongozi wa TCRA SACCOS

Mwenyekiti wa kwanza wa TCRA SACCOS alikua Bw. Richard Kayombo aliyeanza uongozi wake tarehe 8 mwezi wa 11 mwaka 2008.

Mwenyekiti wa pili ni Bw. Erasmo A. Mbilinyi alianza uongozi wake tarehe 20 mwezi wa 4 mwaka 2011.

Mwenyekiti wa tatu ni Bw. Thadayo Ringo aliyeanza uongozi wake mwaka 2021, ambaye anaongoza SACCOS hadi leo.

Meneja wa TCRA SACCOS ni Bw. Martin C. Kahimba.

Maendeleo ya TCRA SACCOS

Historia ya TCRA SACCOS

2008
November, 2008

Kuanzishwa kwa TCRA SACCOS

Kuanzishwa kwa TCRA SACCOS
Takribani miaka miwili tangu kuanzishwa kwa Mfuko wa Kusaidiana Mamlaka ya Mawasiliano (MKM), wajumbe wa MKM waliazimia kuunda chombo cha kiuchumi, TCRA SACCOS.
2011
April, 2011

Usajili wa TCRA SACCOS

Usajili wa TCRA SACCOS
Mchakato wa kuanzisha TCRA SACCOS ulichukua takribani miaka mitatu hadi kupata usajili kwa namba DSR. 1314.
2012
April, 2012

Uchaguzi wa Viongozi wa Awali

Uchaguzi wa Viongozi wa Awali
Mwenyekiti wa kwanza aliyechaguliwa ni Erasmo Anthony Mbilinyi, na makamu akiwa Richard Kayombo.
2014
February, 2014

Mwanzo wa Mikopo

Mwanzo wa Mikopo
TCRA SACCOS ilifanikiwa kupata mkopo wa TZS 500,000,000 kutoka kwa mwajiri, kwa masharti nafuu. Mkopo huo uliiwezesha SACCOS kuanza kutoa mikopo kwa wanachama wake. TCRA SACCOS haijawahi kushindwa kutoa mikopo kwa wanachama wake.

Chati ya Shirika