Jenga.
Kuza Uchumi.
TCRA SACCOS inawezesha wanachama kutimiza malengo yao ya kifedha na kukuza uchumi wa taifa
TCRA SACCOS inawezesha wanachama kutimiza malengo yao ya kifedha na kukuza uchumi wa taifa
TCRA SACCOS ilianzishwa mwaka 2006 ambapo watumishi wa TCRA walikubaliana kuanzisha Mfuko wa Kusaidiana Mamlaka ya Mawasiliano (MKM). Uchaguzi uliitishwa na waanzilishi wa mfuko kwa pamoja walimchagua mwenyekiti wao wa kwanza, Mhandisi James M. Kilaba.
Kifuatacho ni muhtasari wa maendeleo ya TCRA SACCOS kuanzia kipindi cha Desemba 2022 hadi Desemba 2023. Taarifa zilizoainishwa ni kutoka kwenye vitabu vya fedha vya SACCOS (audited financials).
Kiasi cha mikopo kwa wanachama kilipungua kwa kiasi kidogo cha asilimia 1.8 kuanzia Desemba 2022 hadi mwisho wa Desemba 2023.
Akiba ndani ya SACCOS iliongezeka kwa asilimia 8.6 kuanzia Desemba 2022 hadi mwisho wa Desemba 2023.
Amana kutoka kwa wanachama ilipungua kwa asilimia 23.1 kuanzia Desemba 2022 hadi mwisho wa Desemba 2023.
Kiwango cha hisa za wanachama kilipungua kwa asilimia 21.7 kuanzia Desemba 2022 hadi mwisho wa Desemba 2023.