HATUA ZA KUJIUNGA

  1. Maombi ya uanachama yanapokelewa kwa maandishi, kisha kamati itapitia maombi. Ikiwa ombi limekubaliwa, mwanachama mpya atatangazwa kwenye mkutano;
  2. Maombi yatapitiwa ndani ya siku thelathini (30), na mwombaji atajulishwa ndani ya kipindi hicho;
  3. Mwanachama mpya atalipa kiingilio cha shilingi elfu hamsini (50,000), na awe na hisa kumi (10). Kila hisa moja ina thamani ya shilingi elfu ishirini (20,000). Mwanachama mpya anapaswa kulipa kwa mkupuo hisa zote za lazima anapojiunga na TCRA SACCOS;
  4. Kila mwanachama atachangia kiasi cha shilingi laki moja (100,000) au zaidi kila mwezi kama akiba yake.
  5. TCRA SACCOS itakua na orodha ya wanachama yenye maelezo ya wanachama, ambayo huyo mwanachama atasaini kuhakiki kwamba maelezo yake ni sahihi;
  6. Mwanachama atapewa cheti cha hisa akishapata hisa zote anazopaswa kulipia kama inavyosemwa kwenye kanuni za TCRA SACCOS.

FOMU YA KUJIUNGA

Kujiunga na TCRA SACCOS, jaza fomu hapa chini, au pakua fomu kupitia ukurasa wa PAKUA.

Jinsia
MwanaumeMwanamke

Hali ya Ndoa
Nimeoa/-olewaSijaoa/-olewa