HATUA ZA KUJIUNGA
- Maombi ya uanachama yanapokelewa kwa maandishi, kisha kamati itapitia maombi. Ikiwa ombi limekubaliwa, mwanachama mpya atatangazwa kwenye mkutano;
- Maombi yatapitiwa ndani ya siku thelathini (30), na mwombaji atajulishwa ndani ya kipindi hicho;
- Mwanachama mpya atalipa kiingilio cha shilingi laki moja (100,000), na awe na hisa ishirini (20). Kila hisa moja ina thamani ya shilingi elfu hamsini (50,000). Mwanachama mpya anapaswa kulipa kwa mkupuo hisa zote za lazima anapojiunga na TCRA SACCOS;
- Kila mwanachama atachangia kiasi cha shilingi laki tatu (300,000) au zaidi kila mwezi kama akiba yake.
- TCRA SACCOS itakua na orodha ya wanachama yenye maelezo ya wanachama, ambayo huyo mwanachama atasaini kuhakiki kwamba maelezo yake ni sahihi;
- Mwanachama atapewa cheti cha hisa akishapata hisa zote anazopaswa kulipia kama inavyosemwa kwenye kanuni za TCRA SACCOS.
FOMU YA KUJIUNGA
Kujiunga na TCRA SACCOS, pakua fomu ya kujiunga kupitia ukurasa wa PAKUA. Anza kufurahia manufaa ya kua mwanachama wa SACCOS bora Tanzania.