Karibu tena kwenye muendelezo wa kidokezo cha kutufundisha jinsi ya kuandaa andiko la mradi (project proposal) na mpango wa biashara (business plan).

Tunaendelea na vipengele vya kuzingatia kwenye maandalizi ya andiko la mradi (project proposal) na mpango wa biashara (business plan).

Tathmini ya kimazingira

Kama tulivyoeleza awali, mazingira ya kiuchumi, kisiasa na kijamii ndani ya eneo la shughuli, kitaifa au kimataifa vinaweza kuathiri shughuli za kampuni.
Tathmini ya mazingira ina vipengele hivi:

  1. Nguvu, Uwezo na Udhaifu wa kampuni au shughuli: Haya ni yanaihusu kampuni au shughuli moja kwa moja. Mfano wa Nguvu au Uwezo ni weledi na uzoefu wa wahusika, kuanzia mwendeshaji mkiuu au mmilki hadi wafanyakazi. Udhaifu ni kama vile kutokuwa na ujuzi katika maeneo muhimu.
  2. Fursa na Changamoto: Haya ni mambo yaliyoko kwenye eneo la biashara au shughuli. Fursa inategemea aina ya shughuli mhusika anayoifanya. Mfano wa fursa kwa wanaofanya biashara za kupangisha nyumba ni kuanzishwa kwa viwanda vingi na kuongezeka kwa ajira sehemu ambayo mhusika ana shughuli. Changamoto ni mambo yanayoweza kuifanya kampuni au shughuli inayofanyika kutokumudu ushindani kwenye soko la huduma au bidhaa. Utambuzi na uelewa wa changamoto unamwezesha mhusika kubuni njia na mikakati ya kukabiliana nazo.

Wataalamu waliunda kiolezo (template) cha kufanya tathmini hii, kama ilivyoonyeshwa chini.

NGUVU/ UWEZO

Elezea mambo yanayokufanya uweze kufanikiwa. Weka kwa safu (yaani rows); ila yawe kati ya matatu na saba.

UDHAIFU

Mambo yanayokukwamisha. Weka kwa safu; ila yasizidi manne, vinginevyo utamkatisha tamaa mlengwa.

CHANGAMOTO

Za Nje ya mfumo wa kutoa huduma/ bidhaa, kimataifa

Kama ilivyoelezwa juu

FURSA

Zote zilizoko kwa huduma au bidhaa husika

Kwa utaratibu ulioeleza juu.
Hata hivyo unaweza kuweka
fursa nyingi ili kuvutia wahusika.

Malengo ya jumla ya Kampuni au shughuli

Hapa weka malengo unayokusudi kuyafikia kwa kutoa takwimu na kuelea kipindi au muda wa kufikia malengo hayo. Kwa mfano, iwapo unafuga kuku, lengo linaweza kuwa: Kuanzisha kiwanda cha kusindika chakula cha kuku ifikapo Septemba 2022.

Mikakati ya kufikia malengo

Kwa kila lengo utakaloweka, ainisha mikakati ya kulifikia. Vilevile, ainisha shughuli zinazotakiwa kufanyika na namna ulivyojipanga au mlivyojipanga. Vingine vya kuweka ni bajeti na wahusika wa kazi hizo ili kufikia kila lengo husika. Kila lengo liwekwe tofauti.

Vyanzo vya bajeti

Kwa kuwa shughuli itahitaji fedha, elezea chanzo cha bajeti kwa kila shughuli. Unaweza kuandaa jedwali tofauti au kuongezea kipengele cha bajeti kwenye jedwali lenye kila lengo.

Mfumo wa ufuatiaji na kupima matokeo

Kufikiwa kwa malengo kutahitaji usimamizi. Ni muhimu kwa na mfumo wa kufutilia utekelezaji, kutamua changamoto za utekeeaji na kuhukua hatua.
Ufuatiliaji ufanyike kwa vipindi vifupi vifupi, ikiwekana kila wiki au mwezi kutegemeana na ukubwa wa mradi au tarehe za kufikia malengo husika.

Kutambua hatari

Hatari mambo, matukio au vitu vinavyoweza kuathiri shughuli au kampuni kwa kipindi husika. Nyingine zinawea kwa ndani ya kampuni au shughuli unayofanya.
Ni vyema kutambua hatari na kuchukua hatua stahiki kuzuia, kukwepa au kukabiliana na hatari.

Mtiririko wa mapato

Kwa kuwa shughuli au kampuni yoyote inahitaji kupata faida, ni vyema kuonyesha mtiririko wa mapato na fedha, kwenye jedwali mahsusi ambalo linaandaliwa na mhasibu.

Masuala ya jumla ya kuzingatia

  • Hakikisha hakuna makosa ya uandishi au sarufi katika nyaraka utakazoandaa na kuwasilisha. Hii itaonyesha umakini.
  • Shirikisa wataalamu wa kila eneo la shughuli unayoifanya kama utakuwa na shauku kuhusu unachotakiwa kuweka kwenye andiko.
  • Usishirikishe watu wasiohusika na ambao huna mamlaka nao katika kuandaa mpango wa biashara, mradi au andiko lolote ili kuepuka wazo lako kufanyiwa kazi na watu wengine, na pengine kwa uharaka zaidi na hivyo kukukoseha fursa.
  • Kuwa na utaratibu wa kuangalia mazingira (scan) ili kubaini fursa na hatari zinazoweza kuikabili shughuli yako. Usiache fursa kwenye eneo lako la shughuli zikakupita bila kuzifuatilia.

Viambatanisho muhimu

Ni muhimu kuweka vitu vyotote ambavyo ni muhimu kutoa picha kamili ya kampuni au shughuli husika.

Hitimisho

Uandaaji wa maandiko ya kibiashara au miradi ni muhimu ili kuhakikisha kwamba shughuli yako inakuwa na nyaraka muhimu zitakazotumiwa na watakaoridhi uendeshaji wake, na sio lazima kazi hii isubiri wakati wa kutafuta fedha au wabia.
Hapa tumetoa vidokezo kadhaa, lakini kuna vingi zaidi kutegemea na aina ya shughuli unayofanya au kampuni unayoendesha au kusimamia.
Kwa maelezo zaidi, au kwa huduma za kuandaliwa andiko la biashara au mradi, wasiliana na: bgamoyosafarilodge@gmail.com, au simu 0769 111811.

CategoryVidokezo