Rais John Pombe Joseph Magufuli, ambaye alifariki dunia tarehe 17 Machi 2021 alinzisha mipango ya kuinua na kuendeleza shughuli za ushirikika kwenye ngazi zote na kukuza ujasirimali.
Hotuba yake wakati wa kuzindua Bunge la 12 tarehe 13 Novemba 2020 na Ilani ya Uchaguzi ya CCM vimeainisha mipango ya kupanua huduma za kifedha na upatikanaji wa mitaji kupitia mikopo ya masharti nafuu kwa wafanyabiashara wadogo na kwa vikundi vya kuweka na kukopa.
“Tutaimarisha mifumo ya upatikanaji wa mitaji kwa wakulimwa wadogo na wawekezaji kwa kushirikisha taasisi za kifedha, zikiwemo benki”, alisema Mheshimiwa Magufuli Bungeni.
Mipango ya kupanua wigo wa ushikika ni pamoja na kuhamasisha makundi maalum kujiunga na vyama vya ushirika vinavyogusa sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Ilani ya Uchaguzi ya CCM inaelekeza Serikali kuhamasisha kilimo cha mazao-lishe ili kuboresha afya za wananchi.
Mipango ya serikali pia ni kuhamasisha na kuweka msukumo katika kubadili fikra na mazingira ya kilimo kwa lengo la kubadili mtazamo wa uendeshaji wa sekta hii kuwa wa kibiashara zaidi ya wa kujikimu.