bajeti-2021-2022

BAJETI YA 2021/2022 NA WAJASIRIAMALI

Bajeti kuu ya mwaka wa fedha 2021/22 imepokelewa na mapendekezo mengi ya mabadiliko ambayo yanawahusu wafanyabiashara wadogo kama wanachama wa TCRA SACCOS.
Baada ya kuipitia hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dr. Mwigulu Lameck Nchemba, tumeandaa muhtasari maeneo makuu ya kuzingatia wakati huu wa bunge la bajeti.

MABADILIKO YA KODI NA USHURU

Sehemu kubwa ya mabadiliko yatakayotokea ni katika malipo ya ushuru na kodi za wafanyabiashara na waajiriwa.

Badiliko la kwanza ni kwenye ushuru kwa wachimbaji wadogo wa madini ambao mauzo hayazidi TZS Milioni 100 kwa mwaka. Imependekezwa kodi maalum ya mapato ya 3% juu ya thamani ya madini yaliyouzwa. Malipo ya ushuru yafanyike pindi madini yanapouzwa. Hii inasaidia biashara ndogo ambao watalipa ushuru kadri ya mzunguko wao wa fedha.

Ushuru wa Ujuzi na Maendeleo (SDL) utatozwa kwa biashara zenye wafanyakazi zaidi ya kumi (10). Hili ni ongezeko kutoka kiwango cha chini cha wafanyakazi 4. Hatua hii itapunguza majukumu ya mwajiri mdogo. Pamoja na hilo, mchango wa SDL utapunguzwa kutoka 1% hadi 0.6% kwa sekta binafsi.

MISAMAHA YA KODI

 • Msamaha wa VAT kwenye vyumba vya baridi (cold rooms) (HS Code 9406.10.10 and 9406.90.10);
 • Msamaha wa VAT kwenye bima ya ufugaji kwa wafugaji;
 • Msamaha wa VAT kwenye madini ya thamani na madini ghafi yaliyoagizwa kutoka nje ya nchi;
 • Msamaha wa VAT kwenye bidhaa na huduma zote zinazichangia mradi wa East African Crude Oil Pipeline (EACOP);
 • Msamaha wa VAT kwenye mafuta ghafi chini ya HS Code 2709.00.00;
 • Msamaha wa VAT kwenye nyasi bandia chini ya HS Code 5703.30.00 na 5703.20.00 zitakazotumika kwenye viwanja vya mpira wa miguu vya manispaa;
 • Msamaha wa VAT kwenye simu janja, tablets na modemu.

MAPUNGUZO NA MAONGEZEKO

 • Kuondoa VAT kwenye makopo ya kuhifadhi maziwa chini ya HS Code 7310.29.20;
 • Kusamehe VAT kwenye makopo ya maziwa ya aluminium na chuma chini ya HS Code 7310.29.90, 7310.10.00 na 7612.90.90;
 • Kuondoa VAT kwenye taa zinazochaji kwa jua (Solar Lights) chini ya HS Code 85.13 na 94.05;
 • Ondoleo la amana ya ushuru wa 15% wa kuagiza sukari kwa matumizi ya viwandani;
 • Mabadiliko kwenye sheria ya Usalama Barabarani (Road Traffic Act) yatapunguza faini ya makosa ya barabarani ya pikipiki na bajaji kutoka TZS 30,000 hadi TZS 10,000 kwa kila kosa;
 • Punguzo la kodi ya kushinda kwenye Ubashiri wote wa michezo kutoka 20% hadi 15%;
 • Punguzo la gharama ya leseni ya TALA (Tanzania Tourism Business License) kwa wakala wa usafiri kutoka USD 2000 hadi USD 500;
 • Pendekezo la kupunguza gharama ya usajili wa Personalized Plate Number kutoka TZS 10,000,000 hadi TZS 5,000,000 kila miaka mitatu (3);
 • Ushuru mpya wa 10% kwenye pikipiki zinazoagizwa kutoka nje ya nchi zenye umri wa miaka Zaidi ya mitatu chini ya HS Code 871;
 • Pendekezo la kurudisha marejesho ya VAT kwa bidhaa zinazonunuliwa na wanunuzi waliosajiliwa kutoka Tanzania bara na Zanzibar na kinyume chake.

National Environmental Management Council (NEMC)

 • Punguzo la ada ya kuharibu madawa yaliyopita muda salama wa matumizi kutoka TZS 1,000,000 hadi TZS 100,000;
 • Ada ya mazingira inayotozwa kila mwaka kupungua kutoka TZS 200,000 hadi TZS 100,000.

OSHA
Punguzo la gharama ya ukaguzi wa umeme na ada ya ukaguzi wa jumla (general inspection) kutoka TZS 590,000 hadi TZS 150,000.

Jeshi la Zomamoto (Fire and Rescue Force)

 • Ondoleo la tozo ya moto (fire levy) kwa mashamba ya bustani (horticultural farms);
 • Ondoleo la tozo kwa cheti cha Fire Compliance kwa vituo vya mafuta vya mjini na vijijini. Cheti kitatolewa bure baada ya ukaguzi;
 • Ondoleo la tozo ya ukaguzi wa moto kwenye mashamba na boma waliokua wakilipa TZS 100,000 hadi TZS 1,000,000.

Land Rent Act, CAP 113
Punguzo la kiwango cha malipo kutoka 2.5% hadi 0.5% kwa viwanja vipya na 1% hadi 0.5% kurekebisha ardhi (regularizing land).

Property Tax Act, CAP 289
Kodi ya ardhi itatozwa kupitia malipo ya umeme kwenye nyumba zenye mita za TANESCO. Tozo hii itakua TZS 1,000 kila mwezi kwa jingo la kawaida lenye mita moja. TZS 5,000 itatozwa kwa kila ghorofa ya jengo lenye mita moja.

CategoryVidokezo
Write a comment:

*

Your email address will not be published.