Biashara ndogo zinaweza kutumia fursa ya huduma za mtandaoni kufikia wateja wengi zaidi. Kuna njia kuu tatu za biashara kuweza kuwafikia wateja wake mtandaoni.
Tovuti
Tovuti inasaidia biashara kutambulika duniani kote, kwani kila mtu mwenye uwezo wa kutumia simu au komputa ataweza kufikia buashara yako bila kufunga safari. Badala ya kupanda gari ya kkoo, mteja anaweza kupitia tovuti yako, ajue unachokiuza, na kununua papo hapo kwa kutumia miamala ya simu.
Matangazo kwenye blog
Tovuti zinazotumika kurusha maudhui mtandaoni yanalenga wasomaji wa rika tofauti. Hizi blog zinaruhusu matangazo kwenye tovuti zao, ambazo ni fursa nzuri kwa mfanyabiashara kuwafikia wateja wengi zaidi.
Mitandao ya Jamii
Mitandao kama ya Facebook na Instagram imeshamiri sana Tanzania, na wafanyabiashara wameona umuhimu wa kurusha maudhui kwenye hii mitandao. Watumiaji wengi hutafuta biashara kwenye Instagram na huangalia picha zilizorushwa kusaidia maamuzi ya kunuua bidhaa husika. Utafiti umeonyesha kwamba biashara zilizoko kwenyemitandao ya jamii zinapata mauzo 78% zaidi ya wenzao wasiotumia hizi huduma.
Ni muhimu sana kwa wafanyabiashara kutambua fursa inayotokana na kutumia huduma za mtandaoni kukuza wigo wa biashara zao, kukuza mapato yao, na kuridhisha watu wengi zaidi na bidhaa zao.