SACCOs ni tofauti na vyombo vingine vya akiba ya fedha kwa sababu kadhaa. Wanachama wa SACCOs wanaweza kuhifadhi pesa, kununua hisa, na kuchukua mikopo kwa riba nafuu. SACCOs hua na miongozo na kanuni za kawaida na za kipekee kulingana na malengo au makubaliano ya wanachama.

Mazoea ya Kuhifadhi Pesa

Mara kwa mara, watu huwaza kwamba pesa haitoshi. Mahitaji hukua, madeni huongezeka, hata visima vya pesa hukauka. SACCOs inaendekeza mazoea ya kuhifadhi pesa na kuboresha adabu ya pesa ya wanachama, kwani husaidia mwanachama kuona jinsi akiba inavyokua na kuleta maendeleo ya hali ya maisha.

Faida ya Gawio

Kulingana na kanuni za SACCOs, wanachama wanapokea gawio kulingana na hisa walizonunua baada ya kurejesha amana. Gawio hutolewa kila mwaka kulingana na faida iliyopatikana baada ya mikopo na uwekezaji wa pesa ya SACCOs.

Mikopo ya Dharura

Matukio mengi hutokea bila kukusidia. Dharura zinaweza kutuweka katika wakati mgumu tukiwaza mahala pa kupata pesa. Hapo ndipo SACCOs inakupa ahueni na mikopo ya dharura yenye riba ndogo sana.

Dhima ya Mwanachama

SACCOs zinaweza kutumia pesa na mali kufanyia biashara, ambapo kuna uwezekano wa kupata faida na kufilisika. Iwapo biashara imeshindwa kuleta faida na ikafilisika, wanachama hawatalazimika kutumia mali zao binafsi kulipia madeni yoyote yatakayokwepo.

Riba za Mikopo

Mikopo ya SACCOs inavutia wajasiriamali zaidi ya mikopo ya taasisi zingine za kifedha kwa sababu ya riba nafuu inayotozwa na SACCOs, na makubaliano rafiki ya kurejesha amana itakayokuza kiasi cha pesa kinachoweza kukopwa na wanachama.

Kujiunga na SACCOs ni uamuzi wenye manufaa kwa maendeleo ya biashara za wajasiriamali, na hali ya maisha ya wanachama wanaofaidika na huduma za kifedha. Ukitaka kujiunga na TCRA SACCOS, bonyeza hapa kuelekezwa kwenye ukurasa wa kukupa muongozo.

CategoryMiradi, Vidokezo
 1. July 1, 2022

  nahitaji kujiunga na saccos naomba muongozo

  • October 14, 2022

   Tembelea ukurasa wa Kujiunga na SACCOS kwenye sehemu ya Uanachama. Au piga simu namba 022 241 2011

 2. August 2, 2022

  Naitaji kujua utaratibu wa kujiunga yaan kuwa mwachama

  • October 14, 2022

   Tembelea ukurasa wa Kujiunga na SACCOS kwenye sehemu ya Uanachama. Au piga simu namba 022 241 2011

 3. April 10, 2024

  Je mfanya kazi binafisi anaweza kujiunga?

  • June 11, 2024

   Asante kwa swali, hapana, wanachama wa TCRA SACCOS ni wafanyakazi wa TCRA pekee. Blogu hii inatoa taarifa za kuwasaidia wajasiriamali.

Write a comment:

*

Your email address will not be published.