Mambo ya kuzingatia unapotaka kuaandaa andiko la mradi (project proposal) au mpango wa biashara (business plan).

Utangulizi: Staili ya uandishi

Katika kuendesha shughuli zetu za ujasiriamali, kuna wakati tutahitaji kupanua shughuli zetu na hivyo kuhitajika kuomba mkopo au kuingia ubia wa kibiashara na mhusika mwingine. Kwa vyovyote vile, utahitajika kuwasilisha taswira ya shughuli unayoifanya ili kumvutia na kumridhisha unayehitaji kuwa mbia wako au taasisi unayoihitaji ikupatie fedha au nyenzo. Kuna njia na miundotofauti ya kuandaa na kuwasilisha andiko la biashara au la mradi. Wakati wote utahitajita kuzingatia yafuayayo.

1. Urefu wa andiko

Ili kutokumchosha mlengwa, na kuwa na ufasaha katika maudhui unayoweka, ni vyema andiko liwe fupi, kuanzia kurasa nane hadi 12 likiwa limechapwa kwenye karatasi ukubwa wa A4. Unaweza kutumia fonti, yaani aina ya herufi unazopendelea; lakini zisiwe na urembo mwingi. Maandiko mengi ambayo ninayapitia kama Mshauri Mwelekezi na Mhariri ni Times New Roman au Bookman Old Style, fonti ukubwa wa 12, mistari ikiwa imetenganishwa kwa 1.5, ingawaje hata 1.15 inatosha; lakini isiwe chini ya hapo. Unaweza kutenganisha paragrafu kwa kuziweka mbali (spacing) au kuziingiza ndani (indenting) kwa herufi kati ya tatu na tano.

2. Taarifa za kuweka

2.1. Utambulisho wa kampuni yako au shughuli unazofanya. Hii isizidi
paragrafu mbili. Weka taarifa hizi:
2.1.1. Historia fupi ya shughuli/kampuni; yaani illivyoanzishwa na shuguli inazofanya. Mfano: Bagamoyo Safari Lodge ni hoteli iliyoanzishwa mwaka 2018, inayotoa huduma za malazi, vyakula, vinywaji na mikutano kwenye mji wa kihistoria wa Bagamoyo.
2.1.2. Dira (vision) na Dhima (mission) ya shughuli unayofanya. Mfano: (i) Dira yetu ni kuwa mtoa Huduma za usafiri wa mijini mwenye
kupendwa na kuamimiwa zaidi na wateja.
(ii) Dhamira yetu ni kuwaridhisha watumiaji wa huduma zetu na kwa
kuwahudumia kwa weledi mkubwa.

2.1.3. Malengo ya kampuni/shughuli

Elezea kwa ufupi malengo ya kampuni au shughuli unayoifanya kwa miaka mitatu hadi mitano mbele. Usizidi kipindi hicho kwani malengo ya muda mrefu yanaweza kuathiriwa na mabadiliko katika mazingira ya kiuchumi, kisiasa na kibiashara ndani ya eneo unalofanyia shughuli, kitaifa na kimataifa.

Eneo hapa limetumika kwa maana ya biashara au huduma inayotolewa. Kwa mfano usafirishaji wa abiria au uendeshaji wa hoteli.

Uchambuzi huu ni muhimu kutokana na uwezekano wa kubadilika kwa mwelekeo wa huduma na wa watumiaji wa huduma na/ au bidhaa hizo. Hili la mwisho ni muhimu hasa kutokana na mabadiliko makubwa na ya kasi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA). Lengo la kuwa na malengo ya miaka mifupi mifupi ni kuwezesha kampuni au shughuli kupitia upya mipango yake ya biashara kila baada ya vipindi vifupi na kujipanga upya.

2.2. Maelezo mafupi kuhusu mafanikio ya shughuli husika au mambo ambayo kampuni au shughuli imefanya kwa kipindi cha miaka mitatu hadi mitano nyuma. Yaani kama unaandika 2022, weka mafanikio kuanzia angalau 2017.

2.3. Muundo wa kampuni, yaani namna mlivyojipanga kwenye uendeshajiwa shughuli. Kama una wafanyakazi, elezea namna walivyopangwa, na mtiririko wa usimamizi wa shughuli. Hata kama unaendesha shughuli au kampuni hiyo peke yako, ni vyema kueleza namna unavyoshirikiana na wadau wengine; wakiwemo wanaopitia mahesabu yako.

Tathmini ya kimazingira. Kama tulivyoeleza awali, mazingira ya kiuchumi, kisiasa na kijamii ndani ya eneo la shughuli, kitaifa au kimataifa vinaweza kuathiri shughuli za kampuni.

Tathmini ya mazingira ina vipengele viwili vikuu nitakavyoelezewa kwa urefu kwenye nakala ifuatayo. Endelea kufuatilia vidokezo hapa TCRA SACCOS kukuza uwezo wako wa kibiashara.

CategoryMiradi, Vidokezo
  1. October 28, 2022

    Naomba msaada wa andiko mradi wa dagaa pdf

    • December 21, 2022

      Asante kwa ombi lako, maandiko ya miradi yanahitaji uelewa mzuri wa malengo yako kama muandaaji. Unatarajia kuanzisha kiwanda cha kuchakata dagaa, uvuvi wa dagaa, au ukulima wa dagaa? Pitia ripoti iliyoandaliwa na Josephine Mkunda na kuchapishwa kwenye tovuti ya ResearchGate kuhusu biashara ya dagaa eneo la ziwa Victoria kwa ufafanuzi zaidi.

  2. December 8, 2022

    Napenda kujifunza zaid kwani nina wazo ambalo nataka kulifanya na linaniumiza kichwa kwani nawaza wafadhili na jinsi ya kuliandaa likae vizur

    • December 21, 2022

      Kuandaa andiko la mradi au mpango wa biashara ni njia sahihi ya kupata wafadhili wa mradi au biashara yako. Je, ni taarifa gani ungependa kupata ili kukusaidia kwenye haya maandalizi?

  3. June 14, 2023

    Taarifa ni nzuri na inaeleweka

    Asante sana

    • June 11, 2024

      Tunashukuru sana kwa pongezi, asante kwa kusoma

  4. September 18, 2023

    Naomba mawasiliano yenu. Simu namba

    • June 11, 2024

      Unaweza kuwasiliana nasi kupitia 022 241 2011/2. Pia unaweza kutuma ujumbe kwenye ukurasa wa HUDUMA > WASILIANA NASI

  5. September 26, 2023

    Asante kwa elimu nzuri, Ila naomba kupata walau sampuli ya mpango Kazi kuhusianaa na biashara ya mifugo kwa kununua na kuuza ng’ombe

    • June 11, 2024

      Shukrani bwana Felix, kupata andiko la miashara ya mifugo, tunashauri uwasiliane na mabwana shamba (extension officers) wakupe taarifa zaidi kuhusu soko lilivyo na namna ya kuanza ili uepuke changamoto za awali

  6. November 17, 2023

    Naomba kupata andiko la kuanzisha kiwanda kidogo cha kutengeneza viatu vya ngozi, andiko ilo liweze kunipatia wafadhiri kwaajili ya kuanzisha kiwanda cha kijasiriamali Katika upande wa bidhaa za ngozi ikiwemo viatu vya kufunika, buti, mikoba, mabegi na wallet.

    • June 11, 2024

      Kiwanda cha viatu vya ngozi ni wazo zuri sana. Pa kuanzia, ni sahihi kutafuta wataalamu wanaoweza kushna viatu, pamoja na muuzaji wa ngozi halali na imara ili uweze kuunda sampuli kadhaa za kuonyesha uwezo. Tafadhali pitia nakala yetu kuhusu kurusha maudhui mtandaoni kujua namna zingine za kupata ufadhili kupitia wateja wa awali.

  7. February 27, 2024

    Napenda nipate andiko la kuanzisha kampuni ambayo itajihusisha na kilimo. Mazao ambayo ninalima ni kahawa, Parachichi haya Yako Mbinga. Paia nalima Korosho Masasi. Kampuni hiyo ni ya kwangu. Na uzoefu wangu ni Mtaalam wa Kilimo .( Msc degree). Shughuli ni uzalishajo , Uchakataji na pia uuzaji wa mazao ninayozalisha.

    • June 11, 2024

      Asante kwa hili ombi. Tunafanyia kazi nakala mpya itakayosaidia na maelezo ya kilimo cha maparachichi na mazao mengine ya matunda. Unaweza kuwasiliana nasi kuweza kuandaa nakala zingine pamoja nasi kwa manufaa ya wajasiriamali wengine nchini

Write a comment:

*

Your email address will not be published.