Mhandisi Mkuu Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Joel Chacha amefariki dunia tarehe 26 Desemba 2021 akiwa kwenye mazoezi ya viungo nyumbani kwake Dar es Salaam na kuzikwa Tarime, mkoani Mara tarehe 30 Desemba. “TCRA tumempoteza mmoja wa wataalamu wetu mahiri na aliyebobea katika tasnia ya uhandisi wa mawasiliano”, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dr. Jabiri…

Tutakuwa tunawaletea vidokezo muhimu kuhusu masuala ambayo mtu anatakiwa kuyazingatia anapotaka kuanza shughuli za kumuingizia kipato, kwa njia ya kutoa huduma au kuuza bidhaa. Pamoja na kusajili shughuli ya binafsi inayokuingizia kipato kama kampuni yenye dhima ya kikomo (limited liability company), unaweza pia kuisajili kama shughuli yenye umilki wa ubia (partnership) au umiliki wa pekee…

SACCOs ni tofauti na vyombo vingine vya akiba ya fedha kwa sababu kadhaa. Wanachama wa SACCOs wanaweza kuhifadhi pesa, kununua hisa, na kuchukua mikopo kwa riba nafuu. SACCOs hua na miongozo na kanuni za kawaida na za kipekee kulingana na malengo au makubaliano ya wanachama. Mazoea ya Kuhifadhi Pesa Mara kwa mara, watu huwaza kwamba…

BAJETI YA 2021/2022 NA WAJASIRIAMALI Bajeti kuu ya mwaka wa fedha 2021/22 imepokelewa na mapendekezo mengi ya mabadiliko ambayo yanawahusu wafanyabiashara wadogo kama wanachama wa TCRA SACCOS. Baada ya kuipitia hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dr. Mwigulu Lameck Nchemba, tumeandaa muhtasari maeneo makuu ya kuzingatia wakati huu wa bunge la bajeti. MABADILIKO…

Rais John Pombe Joseph Magufuli, ambaye alifariki dunia tarehe 17 Machi 2021 alinzisha mipango ya kuinua na kuendeleza shughuli za ushirikika kwenye ngazi zote na kukuza ujasirimali. Hotuba yake wakati wa kuzindua Bunge la 12 tarehe 13 Novemba 2020 na Ilani ya Uchaguzi ya CCM vimeainisha mipango ya kupanua huduma za kifedha na upatikanaji wa…

Mradi Katika shughuli za kuingiza kipato, Mradi ni shughuli yoyote ile ambayo inabuniwa, kupangwa na kutekelezwa kwa madhumuni ya kupata faida. Ingawaje kimsingi mradi unakuwa na wakati maalumu wa kuanza na kumalizika, kwenye shughuli za biashara mradi unaweza kuendelea kwa kipindi kirefu. Mara nyingi tunapoanzisha shughuli za kutuingizia kipato, tunakutana na istilahi (terms) nyingi ambazo…

Maandalizi ya sera na masharti ya chama kwa ajili ya kuomba leseni yanaendelea.

Mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu za kugombea uongozi ndani ya TCRA SACCOS unaendelea. Wanachama wanaruhusiwa kuwania nafasi katika uchaguzi kwa kujaza fomu ya maombi (Kwa mujibu wa kifungu cha 9 cha jedwali la sheria ya vyama vya ushirika No. 6 ya mwaka 2013).